Wanafunzi wa Secondary ya Dr.A.M.Shein iloyopo kata ya Mpepai katika wilaya ya Mbinga, wamehimizwa kusoma kwa bidii hadi kufikia chuo kikuu. Akiongea na wanafunzi hao, Mkuu wa shule hiyo ndugu Nchimbi amesema kuwa, kila mmoja anapaswa kuwa na kiu ya mafanikio kielimu. "Huyu mwalimu wenu anaendelea na masomo yake katika chuo kikuu cha Dodoma, hivyo nanyi inawabidi kuwa na kiu ya mafanikio ili muweze kumfuata huko UDOM" Alisema ndugu Nchimbi akimrejelea mwalimu wa shule hiyo ndugu Komba Philbert ambaye kwa sasa anasoma katika chuo kikuu cha Dodoma.
No comments:
Post a Comment