Thursday, 12 December 2013

THE BADS OF POPULATION DISPLACEMENT ON THE ENVIRONMENT.

population displacement leads to;
  • deforestation
  •  land degradation;
  •  unsustainable groundwater extraction.
  •  water pollution 
  • destruction of ecosystem
  • NB: Welcome for a discussion of either adding more points, reject the existing by posting yours or 'LIKE' the existing. 

WHY CONTRACEPTIVE USE INEFFECTIVE IN AFRICA?

Ineffective> not achieving what you want to achieve or not having any effects

In Africa; Contraceptive use is higher in Namibia 46% and lower in Senegal 8.7% ( (Nwachukwu and Obasi, 2006-2007).
FACTORS.
  • Extreme poverty, lack of access to birth control, growing population, cultural and religious oppositions, poor quality of available services, gender based barriers, spousal disapproval, low education etc.
  • NB: You can comment this article by adding more points or clashing the existing points

Thursday, 7 November 2013

HIVI NI "BIG RESULTS NOW!" AU "BIG RESULTS NO!"

Hivi juzi tu wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ilitangaza kuondoa zero na kureplace na division five. Hali hiyo ilionekana kama ni njia mojawapo ya kuelekea slogan maarufu ya "BIG RESULTS NOW", kwa bahati mbaya sana maamuzi hayo hayakumaliza wiki, naibu waziri wa elimu alisikika akilijulisha bunge kuwa, division five imefutwa na zero inabaki palepale. Hii pamoja na maana nyingine inaweza ikamaanisha kwamba, maana ya "BIG RESULTS NOW" imekumbwa na majanga na baada ya muda si mrefu inaweza ikabadili jina na kuitwa "BIG RESULTS NO".

Tuesday, 29 October 2013

ADHA YA USAFIRI YAWAKUMBA WANACHUO UDOM

Usafiri kutoka chuoni kuelekea mjini na kutoka mjini kuelekea chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) umekuwa wa shida mithiri ya ule wa kutoka Ubungo kuelekea Mbagala (DSM). Akiongea na mwandishi wetu mmoja wa viongozi wa umoja wa wanafunzi wa chuo kikuu Dodoma ambaye hakutaka jina lake lichapishwe alisema kwamba, uongozi unajaribu kuwashawishi wamiliki wa magari zaidi ili waweze kuwekeza katika usafirishaji abiria na hivyo kuondokana na adha ya usafiri ambayo wasomi hao hukumbana nayo.


Monday, 28 October 2013

NI MWALIMU AU DEREVA YEBO!

Duh! Pole sana mwalimu.
Sura unayoiona hapo juu sio ya dereva yebo, bali ni ya mwalimu ambaye baada ya kuhitimu katika chuo kikuu cha Dodoma Kitivo cha elimu June mwaka huu akaamua kurudi nyumbani na kufanya kazi ya udereva yebo. Kwa bahati mbaya akakumbwa na majanga hayo unayoyaona hapo juu. 
Je, wewe utakapohitimu umepanga kufanya shughuli gani? TAFAKARI, CHUKUA HATUA.........!

TUPENI BOOM, TUNADHALILISHWA UJASINI.

Suala la kokosa boom limemweka pabaya mwanachuo mmoja (jina tunalo) wa UDOM COED baada ya kula chakula wakati hana hela ya kulipa.

"Niache bwana nitakulipa boom likitoka".

Mwanachuo huyo alibaki chini ya ulinzi wa MAMA NTILIE huyo hadi msamaria mwema alipojitokeza na kulipa deni ambalo msomi huyo alikuwa anadaiwa. Ama kweli, " Ukitaka kujua ukali wa mlevi, mwaga pombe yake"

WATOTO WA DR. SHEIN WAHIMIZWA KUJIUNGA UDOM

Wanafunzi wa Secondary ya Dr.A.M.Shein iloyopo kata ya Mpepai katika wilaya ya Mbinga, wamehimizwa kusoma kwa bidii hadi kufikia chuo kikuu. Akiongea na wanafunzi hao, Mkuu wa shule hiyo ndugu Nchimbi amesema kuwa, kila mmoja anapaswa kuwa na kiu ya mafanikio kielimu. "Huyu mwalimu wenu anaendelea na masomo yake katika chuo kikuu cha Dodoma, hivyo nanyi inawabidi kuwa na kiu ya mafanikio ili muweze kumfuata huko UDOM" Alisema ndugu Nchimbi akimrejelea mwalimu wa shule hiyo ndugu Komba Philbert ambaye kwa sasa anasoma katika chuo kikuu cha Dodoma.


BODABODA MARUFUKU UDOM

Usafiri wa pikipiki maarufu kama "BODABODA" Umepigwa marufuku katika maeneo ya chuo kikuu cha Dodoma. Hii imebainishwa na maafisa usalima wachuo. Wakizungumza na mwandishi wa habari hii, wanausalama hao wametoa sababu za kupiga marufuku usafiri huo ni kutokaka na kuongezeka kwa ajili zinazosababishwa na BODABODA hizo. Chanzo cha habari hii kiliweza kushuhudia ajali mojawapo katika maeneo ya CAFELATINO COED.



WANAFUNZI WA BED PPM KUPATA MIKOPO YAO.

Wanachuo wa UDOM ambao majina yao ya fedha za 'meals and accommodation' hazikufika kwa wakati watarajie neema ya kupata fedha zao baada ya siku chache kuanzia leo. hayo yamesemwa na waziri wa mikopo alipokuwa akihojiwa na mwandishi wetu. Hivyo wawe na subira wakati matatizo yao yanafuatiliwa kwa karibu

Sunday, 27 October 2013

KASI MPYA NA ARI MPYA UDOM COED

Kwa mara ya kwanza katika historia ya UDOM COED masomo yaanza mara baada ya chuo kufungua. ama kweli hizi ni dalili njema za "BIG RESULT NOW". Hayo yamebainika baada ya chuo kufunguliwa tarehe 19/10/2013 na masomo kuanza rasmi tarehe 21/10/2013. Kasi inatufanya tuamini mambo kadha wa kadha. Akiwahoji wanafunzi mbalimbali mwandishi wetu alibaini kuwa ule mpango wa "BIG RESULT NOW" huenda ukawa upo katika utekelezaji.